JAB YATOA WITO KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KULINDA MASLAHI YA WAANDISHI
Na Mwandishi Wetu. Wamiliki na viongozi wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi na kulinda maslahi ya Waandishi wa Habari, kwa kuwa usalama wa ajira, malipo ya haki na upatikanaji wa stahiki vina mchango mkubwa katika ubora na uaminifu wa habari zinazowafikia wananchi. Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2026 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Wakili Patrick Kipangula, wakatu akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa…